• Hali ya mama wa Albino aliyeuawa yaendelea vizuri

    Hali ya mama wa mtoto mwenye ulemavu wa ngozi Yohana Bahati (1), aliyetekwa na baadaye kuuawa, inaendelea vizuri katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando BMC.

     Tukio la kutekwa mtoto huyo lilifanywa na watu wawili nyumbani kwa mama huyo, mwanzoni mwa wiki hii katika Kijiji cha Ilelema, wilayani Chato, mkoani Geita.

    Ofisa Muuguzi Msaidizi  Kitengo cha Pua na Masikio (ENT),  Agnetha Mutatembwa alisema jana kuwa mama huyo anaendelea kupata nafuu ukilinganisha na siku zilizopita.

    Katika hatua nyingine, watu wa kada mbalimbali wanaendelea kulaani tukio hilo la kikatili la kuuawa mtoto huyo, kisha mwili wake kukatwa miguu na mikono.

    Wakizungumza jana hospitalini hapo walipomtembelea mama huyo Esther Jonas (30), baadhi ya wasanii wa filamu walisema Serikali lazima ichukue hatua kali kwa wahusika.

    Msanii maarufu kwa jina la King Majuto, alisema kuendelea kuuawa kwa watu wenye ulemavu wa ngozi kumetokana kile alichodai kuwa ni uvivu wa Serikali kufanya kazi.

    “Serikali inatakiwa ichunguze jambo hili kwa umakini. Ni aibu kubwa kwa nchi kuendelea kushuhudia vitendo kama hivi,” alisema na kuongeza:

    “Wahusika wanajulikana, kukaa kimya maana yake ni kujidanganya  na kuacha vitendo hivi kuendelee.”

    Msanii mwingine, Single Mtambalike alisema jamii inatakiwa kuondokana na imani potofu  za kuuwa binadamu kwa misingi ya kupata utajiri kama inavyodaiwa kuwa viungo vya walemavu wa ngozi hutumika kwa kazi hiyo.

    Alisema mauaji yanayoendelea yanapaswa kukomesha na jamii lazima ipaze sauti na kukemea mauaji hayo.
  • 0 comments:

    Post a Comment

    GET A FREE QUOTE NOW

    Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit, sed diam nonummy nibh euismod tincidunt ut laoreet dolore magna aliquam erat volutpat.