Rapper Nikki Mbishi ambaye aliuanza mwaka 2015 kwa kufanya uamuzi
uliowashtua mashabiki wengi wa Hip Hop baada ya kutangaza kuacha muziki,
ametangaza kuachia ngoma mpya wiki ijayo.
Baada ya kuulizwa sababu zilizomfanya abadili uamuzi wake na kuendelea kufanya muziki hizi ndio sababu alizozitoa, “Nimegundua kwamba bado watu wananidai vitu vingi sana ngoja kwanza labda nimalizane nao,” Nikki alisema kupitia 255 ya XXL ya Clouds Fm.
“Nimeona response yao ambao walikuwa positive, nimeona watu wangapi niliwa disappoint nimeona watu wangapi yaani wamepoteza ari yao ya kushabikia muziki, vitu kibao. Kwahiyo wakongwe wenyewe wazee wameongea vitu kibao vimetokea kwahiyo ngoja tuone kinachowezekana.”
Ngoma mpya ya Nikki Mbishi itatoka Jumatano ijayo (March 4) ambayo pia itakuwa ni birthday yake.
0 comments:
Post a Comment