• Rais Kikwete ampa ulaji Katibu TFF


    RAIS Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko ya wakuu wa wilaya wapya 27 lakini katika idadi hiyo jina la Katibu Mkuu wa zamazi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Fredrick Wilfred Mwakalebela limo ndani yake.

    Mwakalebela amepata ulaji huo ambapo sasa anakwenda kuiongoza wilaya ya Wanging’ombe iliyopo Njombe huku mwanahabari Shabani Kissu akipelekwa Kondoa.

    Akizungumza na shaffih Dauda Mwakalebela ambaye alikuwa katibu mkuu wa kwanza katika utawala wa Rais Leodgar Tenga amesema ameishukuru serikali kwa kuona mchango wake kwamba anaweza kuisaidia nchi yake.

    “Kwanza niishukuru serikali kupitia Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete kwa kunioan bado nina mchango wa kuisaidia nchi yangu lakini baada ya hilo nataka kufika katika kibarua changu hicho kujua changamoto zinaziwakabili wananchi wa huko,”alisema Mwakalebela.

    “Nikishafanya utambuzi huo sasa nitaanza mikakati ya kuanza utatuzi kwa haraka nikisaidiana na wananchi wa huko, kikubwa naomba ushirikiano kwa wakazi wenzangu wa Wang’ing’ombe.”
  • 0 comments:

    Post a Comment

    GET A FREE QUOTE NOW

    Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit, sed diam nonummy nibh euismod tincidunt ut laoreet dolore magna aliquam erat volutpat.