Mbrazil huyo mwenye umri wa miaka 23 aliyekuwa akisakwa na klabu za Arsenal,Chelsea na Bayern atajiunga na mabingwa hao wa ulaya baada ya msimu huu kumalizika
Beki huyo alijiunga na wababe hao wa ureno mwaka 2012 na msimu huu ameisaidia timu hiyo kufuzu hatua ya robo fainali kwenye michuano ya klabu bingwa Ulaya.
Aidha Danilo alicheza mechi yake kwanza katika timu ya taifa ya Brazil mwaka 2011 na pia ameisaidia timu hiyo kuibuka na ushindi wa 1-0 katika mechi ya kirafiki waliyocheza dhidi ya Chile jumapili iliyopita.
0 comments:
Post a Comment