Ronaldo ambaye siku tatu zilizopita aliwahukumu Granada kwa kuwafunga mabao 5 katika ushindi wa 9-1 atafikisha idadi ya mabao 300 katika michezo ya ushindani endapo atafunga bao moja kwenye mchezo ambao Real Madrid inacheza dhidi ya Rayo Vallecano .
Ronaldo hadi sasa amefunga jumla ya mabao 47 katika michezo 41 ya michuano mbalimbali na anamzidi mpinzani wake Lionel Messi kwa mabao matatu kwenye ligi ya Hispania .
Historia inaonyesha kuwa Ronaldo amefunga mabao manne kwenye tisa dhidi ya Rayo Vallecano hali inayoonyesha kuwa hatakuwa na wakati mgumu kuzifumania nyavu na kutimiza mabao 300 .
0 comments:
Post a Comment