• VODACOM WAZUNGUMUZIA KIFO CHA MASHABIKI WA SIMBA NA KUTOA POLE KWA WAFIWA

    Meneja Uhusianowa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu akiongea na waandishi wa habari (hawapopichani) wakati alipokuwa akituma salama za rambirambi kwa niabaya kampuni kwa familia za mashabiki watimu ya Simba waliopoteza maisha yao kwa ajali ya gari jana mkoani Morogoro wakiwa safarini kuelekea mkoani Shinyanga kuishangilia timu yao dhidi ya Kagera Sugar.

    Meneja Uhusiano wa Vodacom Matina Nkurlu katika taarifa yake aliyoitoa kwa niaba ya kampuni amesema kuwa msiba huu ni mzito kwa watanzania na wapenzi wa soka kwau jumla.(P.T)

    "Vodacom Tanzania kama mdhamini Mkuu wa Ligi Kuu ya Soka ya Vodacom Tanzania Bara tumeguswa sana na msiba huu na tunatoa pole kwa familia zilizopoteza jamaa zao katika ajali hii natunawaombea moyo wa uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi, vilevile tunatoa pole kwa majeruhi wote wa ajali hii na tunawaombea wapone haraka na kurejea katika hali zao za kawaida", Alisema.

    Ajali hiyo iliyotokea katika eneo la Mkundi katika manispaa ya Morogoro juzi imesababisha vifo vya watu saba na wengine zaidi ya 18 kujeruhiwa.

    Kamanda wa polisi wa mkoa wa Morogoro. Leonard Paul amekaririwa akisema kuwachanjo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa dereva aliyekuwa analiendesha gari hilo.

  • 0 comments:

    Post a Comment

    GET A FREE QUOTE NOW

    Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit, sed diam nonummy nibh euismod tincidunt ut laoreet dolore magna aliquam erat volutpat.