• Marekani imemtaka Rais Mpya wa Tanzania Johne Pombe Magufuli kumaliza mgogoro Zanzibar

    Marekani imeitaka serikali ya Tanzania kuheshimu maamuzi ya raia wa Zanzibar katika uchaguzi wa urais uliopita.

    Akimtumia risala za pongezi rais mpya wa Tanzania John Pombe Magufuli kwa ushindi wake wa uchaguzi mkuu uliopita, waziri wa maswala ya kigeni nchini humo John Kerry amesema kuwa Marekani inaendelea kukerwa na hatua ya kufutilia mbali matokeo ya uchaguzi huo.

    ''Tunautaka utawala mpya kuhakikisha kuwa maamuzi ya raia wa Zanzibar yanazingatiwa na kuheshimiwa'',alisema.

    Hii ni mara ya pili kwa Marekani kuzungumzia hatua ya ZEC kufuta matokeo hayo.

    Amesisitiza wito wa Marekani wa kutofutiliwa mbali kwa matokeo hayo huku akizitaka pande zote kushirikiana kwa lengo la kufanikisha mchakato huo wa kidemokrasia kwa uwazi na amani.

    Wakati huohuo waziri huyo amempongeza rais mstaafu Jakaya Kikwete kwa kufanikisha uchaguzi mkuu uliopita.

  • 0 comments:

    Post a Comment

    GET A FREE QUOTE NOW

    Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit, sed diam nonummy nibh euismod tincidunt ut laoreet dolore magna aliquam erat volutpat.