• Mourinho akubali kutotia guu uwanjani

    Meneja wa Chelsea Jose Mourinho amesema hatakata rufaa tena dhidi ya uamuzi wa kumzuia kuingia uwanjani wakati wa mechi dhidi ya Stoke City kesho Jumamosi.

    Shirikisho la soka la Uingereza lilimwadhibu meneja huyo wa umri wa miaka 52 kwa vitendo vyake kwa marefa wakati wa mechi ambayo Chelsea walishindwa 2-1 ugenini West Ham Oktoba 24.

    Mourinho haruhusiwi kutia guu uwanja wa Britannia lakini atasafiri na timu hiyo na hata atatoa uamuzi kuhusu wachezaji wa kubaki na wa kutolewa uwanjani.

    Alipoulizwa kuhusu iwapo atakata rufaa, amesema: "La hasha. Kwa sababu mechi ni ya kesho na najua matokeo ya rufaa hiyo tayari. Nimeamua kuinua mikono.” amesema Mourinho.

    “Ni ujinga kupigana vita ambavyo tayari unajua kwamba utashindwa.” Kando na marufuku hiyo, Mourinho pia atatakiwa kulipa faini ya £40,000.

    Alipoulizwa anavyohisi kuhusu marufuku hiyo na hali ya kulazimika kutazama mechi akiwa nje, alisema: “Mnajua tu si rahisi. Mnajua kufikiria ninavyohisi.

    "Sina mipango ya kutazama mechi. Labda nikae katika kona moja ya barabara nikiwa na I iPad yangu. Au pengine nisiitazame mechi hiyo hata kidogo. Au labda nitumie live scores (mtandao unaotoa habari kuhusu mechi na mabao moja kwa moja)? Matokeo?"

    Jana Alhamisi, shirikisho la soka la Uingereza lilikuwa limekataa rufaa yake ya kupinga adhabu ya kupigwa marufuku mechi moja na kutozwa faini ya £50,000 kutokana na matamshi aliyoyatoa baada ya Chelsea kushindwa na Southampton Oktoba 3.
  • 0 comments:

    Post a Comment

    GET A FREE QUOTE NOW

    Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit, sed diam nonummy nibh euismod tincidunt ut laoreet dolore magna aliquam erat volutpat.