Msimu huu wa Christmas 2015, Kim Kardashian anaziteka headlines kwenye pages mbalimbali za social media na websites za Marekani baada ya tweets zake kupitia page yake ya Twitter kugusa watu wengi.
Siku mbili zilizopita, Kim Kardashian alikuwa anatazama TV nyumbani kwake na ndipo alipokutana na stori ya msichana mmoja anayejaribu kukusanya pair 1000 za viatu ili kuwasaidia watoto wa shirikia la watoto yatima, Soles for Souls… shirika ambalo lilimsaidia msichana huyo kipindi cha mafuriko ya mvua za Katrina.

Baada ya kuguswa na stori hiyo, Kim Kardashian akaona itakuwa jambo zuri kwa familia yake kutoa mchango wao na ndipo alipoingia twitter na kuomba watu wamsaidie kumtafuta msichana huyo kwani yeye na Kanye wapo tayari kumsaidia kufanikisha lengo lake kwa kumpatia pair hizo