• Magufuli aongoza Watanzania kufanya usafi

    Raia nchini Tanzania wameungana na maafisa wa serikali kuitikia wito wa Rais John Magufuli wa kutumia Siku ya Uhuru kufanya usafi.

    Mamia ya watu walirauka na kuanza kusafisha baadhi ya maeneo ambayo hujulikana sana kwa kuwa na uchafu na taka kwa wingi.

    Maafisa wa serikali wanasaidiana na raia
    Wengi wamefurahia agizo la Rais.
    Magufuli aamua Siku ya Uhuru iwe siku ya kazi
    Maoni ya raia Tanzania kuhusu usafi Siku ya Uhuru
    Mwandishi wa BBC Tulanana Bohela anasema Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pia amefika soko hilo la Kariakoo.

    Rais John Magufuli naye amekuwa kwenye aneo la ufuo wa bahari karibu na ikulu akiwa amevalia glavu.

    Katika eneo la Mwenge, wananchi pia wanajizatiti kufanya usafi. Mwandishi wa BBC Regina Mziwanda amewapata wananchi hawa wakiteketeza takataka baada ya kuzikusanya pamoja.
    Taka

    Alipokuwa akitangaza kubadilishwa kwa utaratibu wa kusherehekea Siku ya Uhuru mwaka huu, Rais Magufuli alisema hatua hiyo italiokolea taifa pesa nyingi ambazo hutumiwa katika maandalizi na kufanikisha sherehe hizo.

    “Fedha zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya sherehe hiyo sasa zitumike kwa shughuli zingine za kijamii ikiwa ni pamoja na kupambana na maradhi hasa kipindupindu, kununulia dawa za hospitali, vitanda vya hospitali n.k. kadri kamati za maandalizi zitakavyoamua,” alisema.

    Hata hivyo aliongeza kuwa sherehe hizo zitaendelea kuadhimisha kila mwaka kama kawaida kuanzia mwaka ujao.
    Sikukuu hiyo huadhimishwa kila Desemba 9.

  • GET A FREE QUOTE NOW

    Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit, sed diam nonummy nibh euismod tincidunt ut laoreet dolore magna aliquam erat volutpat.