• Tanesco yaanika deni la bilioni 600/-

    Shirika la Umeme nchini (Tanesco), linadaiwa zaidi ya Sh. bilioni 600 huku likiwa linazalisha kiasi cha Sh. bilioni 100 kwa mwezi, imeelezwa.

    Hayo yalibainishwa jana jijini Dar es Salaam na Kamishna wa Nishati na Maendeleo ya Petroli wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Hosea Mbisse, wakati akifungua mkutano wa siku mbili na wawekezaji wa sekta hiyo kutoka nchi mbalimbali dunia ikiwamo Marekani na China waliokuja nchini kwa lengo la kuangalia fursa zilizopo na namna serikali ilivyojipanga kuhakikisha inakuwa na umeme wa kutosha.

    Alisema licha ya shirika hilo kudaiwa kiasi hicho cha fedha, pia lenyewe linadai wateja wake kiasi cha zaidi ya Sh. bilioni 300.

    “Mpaka sasa Tanesco imejitahidi kuanza kupunguza deni kwa kulipa kiasi cha Sh. bilioni tatu kwa kila kampuni ili kumaliza deni hilo kuanzia mwaka jana na tunatarajia kulimaliza ifikapo 2025,” alisema Mbisse.

    Alibainisha kuwa kuhusu deni wanalodaiwa na mashirika mbalimbali, tayari hazina wameshaanza kufuatilia madeni hayo na kukusanya kiasi cha Sh. bilioni 114.

    “Tuliishirikisha hazina ambayo ilianza kuyakata mashirika hayo fedha ambazo Tanesco inadai na kusaidia kupata kiasi hicho,” alisema.

    Kuhusu uzalishaji alisema Tanesco ina uwezo wa kuzalisha kiasi cha umeme wa Megawatt 650 na kwamba malengo ya serikali ni kufikia kiasi cha Megawatt 10,000 ifikapo 2025.

    “Lengo letu ni kuondoka hapa tulipo kwa kuwa na asilimia 30 ya Watanzania wanaotumia umeme hadi kufikia asilimia 70 katika kipindi cha miaka 10 ijayo,” alisema Mbisse.
    Chanzo: NIPASHE
  • GET A FREE QUOTE NOW

    Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit, sed diam nonummy nibh euismod tincidunt ut laoreet dolore magna aliquam erat volutpat.