![]() |
Trump anaongoza kwenye kura za maoni miongoni mwa wagombea wa Republican |
Trump anasema utafiti uliofanywa hivi karibuni unaonesha kuwa Waislamu wengi wamepandikiza chuki juu ya Marekani na sasa mpaka uongozi ubaini sababu za kuwepo kwa chuki hiyo, watu wanahitaji kujilinda.
Ikulu ya Marekeni imesema tamko la Trump linaenda kinyume na maadili ya taifa la Marekani na maslahi ya usalama wa taifa.
Tamko hilo la Donald Trump limekuja siku chache baada ya watu kumi na nne kuuwawa katika shambulio la risasi zilizopigwa katika mkusanyiko wa watu na wanandoa ambao ni Waislamu.
Trump ashutumiwa kwa kupanga kufurusha wahamiaji
Trump: Dunia ingekuwa bora na Gaddafi na Saddam
Shirika la kijasusi la Marekani FBI limesema Syed Farook na Tashfeen Malik walipandikizwa itikadi kali lakini hawajui na nani na ni kwa namna gani.
Wote wawili waliuwawa na polisi.
FBI walioko California, wameivamia nyumba inayoshukiwa kuhusika katika shambulio hilo na kusema imepata mabomba kumi na tisa ambayo yangeweza kutumika kutengenezea mabomu katika nyumba yao iliyoko Redlands huko California.
Vyombo vya habari vya Marekani vinasema nyumba hiyo ni ya rafiki ambaye anaaminika kuwa alifanya manunuzi ya bunduki zilizotumika katika shambulio
Chanzo:BBC