Akihutubia taifa siku moja baada ya shambulizi hilo,rais Kenyatta amesema kuwa serikali yake itawachukulia hatua kali waliotekeleza shambulizi hilo.
Amasema kuwa waliopanga na kufadhili shambulizi hilo wako katika jamii na kwamba serikali itapata habari ya wahusika ili kukabiliana na wahalifu hao.
Amewataka wazazi,viongozi wa kidini pamoja na wale wa kisiasa kuchukua jukumu kufuatia vijana kupewa mafunzo ya itikadi kali na kwamba serikali yake haitakubali uongozi wa kidini kuanzishwa nchini Kenya na kuongezea kuwa atatea sera za kidemokrasia za taifa kwa gharama yoyote ile.
Chanzo; BBC

0 comments:
Post a Comment