Mwimbaji kutoka Marekani Adele anakabiliwa na kesi ya kuiba wimbo wa msanii kutoka Turkey anayefahamika kama Ahmet Kaya. Msanii huyu anasema wimbo wa Adele ‘Million Years Ago, kutoka kwenye album yake mpya ya ’25’ umefanana kabisa na wimbo wa miaka ya 80 wa msanii Ahmet Kaya unaoitwa Acilara Tutunmak (or Clinging to Pain).
Wimbo huu ulifanyika mwaka 1985 na msanii huyu alifariki miaka 15 iliyopita.
Kwa mujibu wa BBC, mke wa msanii huyu Gulten Kaya amesema haya kuhusu tuhuma hizo “It is unlikely that she would do such a thing. However, if she consciously did it, then it would be theft,”.