![]() |
Wanajeshi wa Nigeria wanaendelea na mashambulizi yao dhidi ya dhehebu hilo la kishia kwa siku ya 3 mfululizo. |
Vuguvugu la kiislamu nchini Nigeria (IMN) linadai kuwa Zeenat Ibraheem ameuwawa kwa pamoja na mwanaye Sayyid Ibraheem Zakzaky.
Sheikh Zakzaky alikamatwa na wanajeshi waliozingira nyumba yao kufuatia madai kuwa wanachama wa kundi hilo walijaribu kumuua kamanda mkuu wa jeshi Jenerali Tukur Buratai huko Zaria siku ya Jumamosi.
Mke wa kiongozi wa kishia nchini Nigeria Sheikh Ibrahim Zakzaky ameuawa na jeshi la taifa
Hata hivyo, kundi la IMN limekanusha madai hayo na kulaumu jeshi kwa kuwauwa zaidi ya wanachama 20 wa kundi hilo, katika makabiliano makali huko Zaria.
Vuguvugu hilo la kiislamu nchini Nigeria linapinga kundi la jihad la waislamu Wa-Sunni la Boko Haram, lakini limekuwa likikabiliana mara kwa mara na jeshi la taifa hilo.
Wakati huohuo, wanajeshi wa Nigeria wanaendelea na mashambulizi yao dhidi ya dhehebu hilo la kishia kwa siku ya 3 mfululizo.
Ripoti zinasema kuwa madhabahu makubwa zaidi ya dhehebu hilo la kishia yameharibiwa na wanajeshi hao.
Ripoti zinasema kuwa madhabahu makubwa zaidi ya dhehebu hilo la kishia yameharibiwa na wanajeshi hao.
Aidha nyumba ya kiongozi wa kishia nchini Nigeria Sheikh Ibrahim Zakzaky imebomolewa.
Jeshi halijajibu madai dhidi yake.
Chanzo: BBC